Kila nchi ina sheria na taratibu zake za namna ya kudhibiti uhalifu, udhalilishaji na namna yoyote ya uvunjifu wa sheria ama taratibu hizo huwa na adhabu kali kulingana na uzito na ukubwa wa kosa lililofanywa ambapo kwa Tanzania yapo makosa ya hadi adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.
Unaambiwa hii ni sheria ya Yemen ambako mtu mmoja alikutwa na hatia ya kubaka na kumuua msichana wa miaka mitatu ambapo adhabu yake ilikuwa kuuawa hadharani watu wakishuhudia.
Mtu huyo alifahamika kwa jina la Muhammad al-Maghrabi ambaye alikuwa na umri wa miaka 41, alipigwa risasi tano mgongoni na Polisi akiwa amefungwa mikono nyuma na kulazwa chini ambapo kabla ya kutekelezwa adhabu hiyo, mtuhumiwa alisindikizwa na Wanajeshi wenye silaha na baada ya tukio hilo walining’iniza maiti juu ili iwe fundisho kwa wengine.
SHAMBULIZI LA CHUI: Majeruhi asimulia alivyonusurika kuuawa
MBUNGE MSUKUMA TENA!! Ni kuhusu maiti iliyookotwa GGM…tazama kwenye hii video hapa chini!!!