Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Jumatatu ya September 4 2017 imefanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza ulipofikia mfumo wao mpya wa uendeshwaji wa club, wanakaribia kuingia siku za usoni baada ya wanachama wao kuridhia mfumo wa mabadiliko.
Simba SC baada ya kukamilisha hatua ubadishaji wa katiba yao, leo imetangaza kuunda kamati ya watu watano watakaosimamia uuzwaji wa hisa za club, wanaounda kamati hiyo ni Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu, wakili Damas Ndumbaro, Abdulrazaq Badru, Yusuph Maggid Nassoro na Thomas Mihayo.
“Kamati ya utendaji baada ya kutafakari imeamua kuunda kamati itakayosimamia mchakato wa wa zabuni wa kumpata muwekezaji au wawekezaji ambao ni wanachama wa Simba ambao watakaonunua asilimia 50 ya hisa za Simba, kamati itakuwa huru”>>> Haji Manara
“Muwekezaji au wawekezaji watakaofanikiwa kuchukua asilimia 50 ya hisa za Simba, haruhusiwi yeye au jamaa yake na familia yake kuingia katika mgawanyo wa zile asilimia 40 zitakazobakia kwa ajili ya kuuzwa kwa wanachama, kipaumbele cha hiyo asilimia 40 ni kwa wanachama waliyogawana asilimia 10”>>> Haji Manara
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0