June 22, 2017 President Magufuli alikamata Headlines baada ya kutoa tamko akiwa ziarani Pwani kuwa katika Serikali ya Awamu ya Tano hakutakuwa na mwanafunzi aliyepata ujauzito akiwa shule kuendelea na masomo baada ya kujifungua.
Tamko hilo liliibua hisa tofauti kwa wadau mbalimbali hasa watetezi wa haki za wanawake na watoto wa kike wakisema inawanyima watoto wa kike haki ya kupata elimu kwa sababu wengi wanaopata ujauzito wakiwa shuleni hawakusudii bali wengine hubakwa.
Ayo TV na millardayo.com zinaye Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko ambaye ni mmoja wa wadau wanaofanya jitihada kumlinda mtoto wa kike na kuhakikisha anapata elimu na amekuwa na hisia tofauti na tamko la Rais JMP.
>>>”Inawezekana Rais Magufuli anatamka kabla hajashauriana na watendaji wake kupata picha halisi ya kinachoendelea Tanzania na madhara ya watoto wa kike.
“Mtoto anaweza kupata ujauzito kutokana na umbali ambapo hukutana na vishawishi; anaweza kubakwa na kushawishiwa kwa sababu ya umbali anaotembea…namuomba Rais Magufuli afikirie tena. Unaweza kukitamka kitu baadaye ukakitafakari ukapata mawazo ya aina mbalimbali.” – Ester Matiko.
ULIPITWA? “Hakuna mwenye mimba atakayerudi shuleni” – Rais Magufuli…tazama kwenye hii video hapa chini!
UZINDUZI! Ni ule mpango wa huduma ya afya bure kwa Wazee