Baada ya winga wa Azam FC Joseph Kimwaga kuumia goti wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu katika Veta Mtwara kuelekea game ya Azam FC dhidi ya Ndanda FC, uongozi wa Azam FC walimsafirisha hadi Afrika Kusini kufanyiwa matibabu.
Joseph Kimwaga ameenda Afrika Kusini na kufanyiwa uchunguzi kutokana na kuumia goti lake la kushoto, hivyo baada ya uchunguzi atafanyiwa upasuaji ambao utamuweka nje akiuguza jeraha lake kwa kipindi cha miezi minne.
Taarifa kutoka kwa Dr Mwanandi Mwankemwa wa Azam FC
“TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU JOSEPH KIMWAGA KUBASHA Kuzaliwa 11/11/1996
Awali ya yote tunamshukuru mwenyezi Mungu mchezaji alisafirishwa salama nakufika salama Ijumaa 1/1/2017″
“Alionwa Jumamosi 2/9/2017 na Dr Nicolas Vincent Palloti Hospital, Pine Lands Cape Town RSA, Jumatatu 4/9/2017 alifanyiwa vipimo na kuthibitika amechanika Meniscus upande wakati(meniscus mfano wake tunautoa kwa mafundi unapofunga nati unaweka washeli kwanza halafu ndio unakaza nati juu yake”
“Mwenyezi Mungu amemuumba binadamu na hiyo washeli inayoitwa meniscus ipo katikati ya goti kuimarisha goti ipo upande wa kati na pembeni hebu gusa sikio lako pembeni miniscus inafananishwa au kulinganishwa na kuta za sikio lako)”
“Ameumia mtulinga wa kati ACL =anterior cruciate ligament .Hivyo basi panapo majaliwa Kimwaga atalazwa jumatano 6/9/2017 saa Tisa alasiri,atafanyiwa upasuaji athroscopy 7/9/2017 atatoka hospital 9/9/2017 ,Atarudi Tanzania 13/9/2017 saa 12 jioni uwanja wa ndege mwalimu nyerere”– Dr Mwanandi
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0