Saa chache baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya (IEBC) kutangaza wajumbe wapya katika Tume hiyo ambao watashughulikia masuala mbalimbali ya Tume katika Uchaguzi wa marudio, Muungano wa Jubilee, kupitia kwa Katibu Mkuu wake Raphael Tuju, umetoa taarifa kuwakataa wajumbe hao waliotangazwa Jumatano na Mwenyekiti Wafula Chebukati.
Katika barua yao, Chama hicho kimekiri kuheshimu Tume hiyo na kutambua changamoto inazozipata lakini hakijakubaliana na orodha ya wajumbe walioambatanisha majina yao.
Sehemu ya barua hiyo ilisomeka; “Tumatambua umeanzisha timu ya mchakato…pia tunathamini hali ngumu mnayopitia lakini tumepata taarifa kuwa katika orodha ni watu wanaojulikana ni wanachama.”
Katika barua hiyo kuliambatanishwa na majina na kusema hawataki watu hao wawepo kwenye Tume hiyo kwa ajili ya kushughulikia Uchaguzi wa marudio.
ULIPITWA? Tamko la CUF ya Maalim Seif kuhusu wabunge 7 walioapishwa jana