Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, Jamal Malinzi na wenzake imeahirishwa hadi September 21, 2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya Wakili wa Serikali, Faraj Ngokah kueleza upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Wilbard Mashauri ana udhuru.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi September 21, 2017.
Washitakiwa wengine ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.
“Sikuja kutafuta Mchumba, nimekuja kufanya kazi za Watanzania” – Rais Magufuli