Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Simon Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na Makamishna na Ma-IGP wastaafu kujadili mambo mbalimbali kuhusu usalama wa raia na mali zao.
IGP Sirro amesema kuwa mkutano huo ulikuwa na lengo la kuelezana na kubadilishana mawazo kuhusu utendaji wa kazi.
Akizungumza baada ya kikao hicho, IGP Mstaafu Omar Mahita amesema miongoni mwa mambo waliyoyajadili ni pamoja na changamoto zinazolikabili Jeshi la Polisi ikiwa ni pamoja na kushughulika na wanasiasa.
>>>”Changamoto zipo nyingi katika Jeshi la Polisi, lakini niwe muwazi kubwa ni namna ya ‘ku-deal’ na wanasiasa kwani ni kazi sana, lakini nafikiri tutaenda tu katika mikakati tuliyojiwekea.” – IGP Mstaafu Omar Mahita.
BREAKING: Watu 30 na Magari wakamatwa Dodoma, Dereva wa Lissu aitwa