Club ya Azam FC usiku wa September 15 2017 ilikuwa mwenyeji wa club ya Kagera Sugar ya Kaitaba Bukoba na kucheza mchezo wao wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi.
Azam FC waliingia uwanjani kuikaribisha Kagera Sugar ambayo haijashinda mchezo wowote wa Ligi Kuu Tanzania bara toka kuanza kwa msimu wa 2017/2018, wakati Azam FC wao walikuwa wanaingia kucheza mchezo huo wakiwa tayari wamepata ushindi game mmoja na sare moja (0-0) dhidi ya Simba.
Mbaraka Yusuph ambaye alijiunga na Azam FC msimu huu akitokea Kagera Sugar, ameiadhibu club yake ya zamani kwa kufunga goli la ushindi dakika ya 43 baada ya kutumia vyema pasi ya Yahaya Zayd na goli hilo kudumu kwa dakika zote 90 na game kumalizika kwa 1-0.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0