Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo September 17, 2017 kupitia kwa Waandishi wa Habari ametoa hotuba kwa Watumishi wa Idara mbalimbali pamoja na Wananchi wa Dar es Salaam ambapo moja ya mambo ameyagusia ni pamoja na kupunguza bei ya viwanja kwa watumishi wa umma.
Katika hotuba hiyo, RC Makonda amesema kila Mtumishi anayefanyakazi kazi chini ya Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam atapatiwa kiwanja cha ujenzi wa nyumba za makazi ya kudumu kwa gharama ya square mita moja kwa Tsh. 4,000 badala ya Tsh 15,000 ambapo kwa ambao hawatokuwa na uwezo wa kulipa kwa mkupuo mmoja watalipa ndani ya miaka mitano huku watumishi wakiruhusiwa kujenga na kulipa taratibu ndani ya miaka mitano na vibali vya ujenzi vitatolewa bure na kupewa kipaumbele.
Press ya kwanza ya Paul Makonda baada ya kumalizana na Wahariri
RC Makonda kasitisha bomoabomoa ya zaidi ya nyumba 17,000