Wanajeshi takribani 21 wa Jeshi la wananchi Tanzania ‘JWTZ’ waliokuwa wamejiunga na chuo cha DIT kwa ajili ya mafunzo ya miezi miwili ya Tehama leo wamehitimisha mafunzo hayo.
Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea ujuzi wanajeshi hao katika mfumo wa teknolojia ya mawasiliano ili wasaidie katika kuimarisha mifumo ya mawasiliano katika jeshi ukizingatia kumekua na uhitaji mkubwa wa teknolojia ya mawasiliano katika sekta mbalimbali.
Ulipitwa na hii? Kituo cha Haki za binadamu wazungumza hali ya ulinzi na usalama nchini