Siku kadhaa zilizopita palikuwa na taarifa ziliripotiwa kuhusu ng’ombe 1,000 kukamatwa wakidaiwa kuingia kwenye hifadhi huku wananchi wa kijiji cha Ololosokowani katika Wilaya la Ngorongoro, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji Kerry Dukanyi wakiiomba Serikali kuingilia kati upigaji mnada wa ng’ombe 630 bila kufuata taratibu wakidaiwa tu kuingia kwenye hifadhi.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ambaye amesema, awali ng’ombe hao walikamatwa baada ya kuingia kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kutolewa bila athari yoyote na wananchi wakatakiwa kutowarejesha tena.
>>>”…wakawarudisha tena hao ng’ombe ndani ya Hifadhi na walipokamatwa tena mara ya pili wale watu waliopeleka hao ng’ombe walishtakiwa na ng’ombe wao walikamatwa kama ushahidi. Process ya Mahakama ikishaanza inaondoka Maliasili inaenda Mahakamani.” – Waziri Maghembe.
ULIPITWA? “Walitishia kutupiga risasi wakachukuwa ng’ombe wetu” – Wanakijiji