Leo September 25, 2017 benki ya CRDB imemuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwenye kampeni ya ujenzi wa ofisi za kisasa za walimu kwa kutoa kiasi cha shillingi milioni 200 ambapo leo wameanza kwa kukabidhi hundi ya shilingi milioni 100.
Akipokea hundi hiyo RC Makonda amesema fedha hizo zitasaidia kununua mifuko 20,000 ya saruji itakayosaidia kufyatua matofali 560,000 ambayo yatajenga ofisi 88 za walimu.
Ameishukuru Bank ya CRDB kwa kuamua kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo ya kuhakikisha walimu wanafanya kazi katika mazingira mazuri yatakayowapa morali ya kufundisha.
Hii je? Nyumba nyingine zaidi ya 100 zateketezwa Kagera
Hii je? Serikali, Wadau wa Ujenzi wakutana