Umoja wa Wazee Mkoa wa Kagera umetoa tamko lao juu ya utendaji wa Rais Magufuli kwa miaka miwili tangu alipoingia madarakani mpaka baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kupitia kwa Mwenyekiti wa Umoja huo, Joseph Masabara wamempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kupambana na ufisadi katika Taifa ikiwa ni pamoja na mpango wa kuiendeleza Tanzania kiuchumi kupitia viwanda.
Aidha Masabara amesema Tanzania imepata umaarufu mkubwa Afrika kupitia uongozi wake na jitihada anazozionyesha ambapo hata wanapotembelea nchi jirani na magari ya Tanzania huitwa Magufuli na kuwataka Watanzania kumuunga mkono kwa kumuombea ili aendeleze mapambano dhidi ya ufisadi.
“Wastaafu wengine hawachoki kusema, wanawashwa” – Rais Magufuli