Leo September 29, 2017 dunia ikiadhimisha Siku ya Moyo, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imetoa huduma ya kupima moyo bure kwa watu wote wanaohitaji huduma hiyo.
Pia madaktari wa taasisi hiyo wametoa elimu ya jinsi ya kufahamu dalili za magonjwa ya moyo ili kwamba wawahi hospitali kuchunguzwa na kupewa tiba pindi wanapohisi kupitia dalili hizo.
Imeelezwa kwamba watu wengi hufika hospitali ikiwa matatizo ya moyo waliyonayo yakiwa kwenye kihali mbaya jambo linalofanya matibabu yake yawe gharama ya juu zaidi na mara nyingi hugharimu maisha ya wagonjwa hasa wasio na uwezo wa kuyamudu.
Ulipitwa na hii? GOOD NEWS!! Huna haja ya kwenda nje kutibiwa Moyo, Tanzania pia wanatibu