Naibu Spika Dr Tulia Ackson ameendelea kuandika historia kubwa kwa jamii baada ya kutimiza ahadi yake ya ujenzi wa choo katika Hospitali ya Rungwe, Mbeya baada ya kukuta changamoto hiyo siku kadhaa zilizopita ambapo wazazi walikuwa wakijisaidia katika mazingira mabovu ambapo ujenzi umegharimu zaidi ya Tsh Milioni 50.
“Hospitali hii ya Rungwe ni kongwe lakini imekuwa na changamoto ya miundombinu, inawagonjwa wengi kuliko miundombinu iliyopo, sisi tulipata fursa ya kupita hapa miezi mitatu iliyopita na kukuta wakinamama wote wanaojifungua wakitumia choo kimoja”-Dr Tulia Ackson
“Sisi kama taasisi ya Tulia Trust baada ya kuliona hilo tukalazimika kuongea na wadau mbalimbali kwa ajili ya kusaidiana kufanya ujenzi huu wa choo ikiwa ni mwendelezo wa kuboresha miundombinu ya elimu na afya nchini ”-Dr Tulia Ackson
“Kwa upande wa afya tuliahidi pia kujenga hiki choo cha wakinamama katika hii hospitali ambacho kimetumia zaidi ya shilingi milioni hamsini, lengo letu ni kuhakikisha ndugu zetu hawa wanakuwa katika mazingira salama”-Dr Tulia Ackson
Full video tamari nimekuwekea hapa chini…
Dr Tulia, Naibu Waziri Wambura walivyofunga Tamasha la Ngoma za Jadi, Mbeya
NOMA !!!! MWANAMKE MPIGA DANADANA MBEYA