Kampuni ya kutengeneza magari ya Nissan imeuzindua kiti cha gari chenye uwezo wa katambua jasho la binadamu ambaye anaendesha gari hilo na kutoa taarifa kama dereva huyo yuko kwenye hatari ya kusababisha ajali kutokana na kupungukiwa na maji mwilini.
Utafiti uliofanywa na taasisi za European Hydration Institute na Loughborough University uligundua kuwa madereva wanaoishiwa na maji mwilini huwa na makosa ya barabarani mengi kama tu ilivyo kwa madereva wanaoendesha wakiwa wamelewa na hii huongeza hatari ya kupata ajali..
Teknolojia hiyo inayojulikana kama Soak, itakua inabadilisha rangi ya kiti hicho pamoja na usukani na kisha kutoa taarifa hiyo na kwamba lengo kuu la teknolojia hii mpya ni kupunguza ajali za barabarani.
Ulipitwa na hii? Fursa nyingine waliyoitoa ubalozi wa Marekani kwa Watanzania