Leo October 4 2017 Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amefika makao makuu ya Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa kwa mara ya pili kwa ajili ya kupeleka ushahidi mwingine ambao anadai kuwa madiwani 10 waliohama CHADEMA wamepewa rushwa.
Baada ya kutoka TAKUKURU, Mbunge Nassari alipata nafasi ya kuzungumza na wanahabari ….>>>“Tumefanya mahojiano, tumefungua jalada rasmi kwa hiyo wao wanaendelea na kazi yao, ushahidi ni mkubwa mno unahusissha watu wengi na matukio ambayo nimekuwa nikiyatunza kwa muda mrefu”
Kauli ya Nassari, Lema na Msigwa baada ya kufikisha ushahidi TAKUKURU, Bonyeza play hapa chini kutazama