Kimbunga kimeendelea kuleta maafa kwa miji mbalimbali Marekani ambapo watu 20 wameripotiwa kupoteza maisha katika miji ya Costa Rica kufuatia Kimbunga Nate huku kikielekea Kaskazini mwa Marekani.
Imeelezwa watu takriban 400,000 hawana maji na maelfu wengine wameachwa bila makazi kutokana na kimbunga hicho ambacho kimesababisha mvua kubwa, maporomoko ya ardhi na mafuriko.
Barabara nyingi hazipitiki, madaraja yameporomoka na pia kimesababisha uharibifu mkubwa kwenye nyumba za watu na majengo. Hali ya dharura imetangazwa katika mataifa kadha ya Amerika ya Kati ambapo watu zaidi ya 20 bado hawajulikani walipo.
Ulipitwa na hii? OLDUVAI GORGE: Mtaalamu kaeleza NYAYO za binadam wa kwanza zilivyopatikana