Alfajiri ya October 6 2017 michezo ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kwa bara la America ilichezwa kama kawaida, kwa upande wa Brazil ambao wao wameshafuzu walicheza game yao ya kukamilisha ratiba dhidi ya Bolivia na wamesalia na michezo miwili.
Brazil walicheza game hiyo ugenini nchini Bolivia katika uwanja wa Hernando Siles lakini changamoto kubwa kwa wachezaji wao ilikuwa kucheza katika sehemu ya hali ya hewa ya nchi ya Bolivia kuwa ndogo (Oxygen) kulingana na game kuchezwa umbaliwa futi 11,900 kutoka usawa wa bahari.
Baada ya dakika 90 za game kumalizika kwa sare tasa (0-0) wachezaji wa Brazil ambao ni wageni kucheza katika eneo la hali ya hewa la namna hiyo iliwalazimu kila mchezaji kupumua kwa kutumia mtungi maalum wa gesi ya Oxygen kutokana na mwili kuhitaji hewa nyingi.
Game ilichezwa katika uwanja wa Hernando Siles mjini La Paz na baada ya game nahodha wa Brazil Neymar alieleza kuwa ni ngumu kucheza katika hali ya hewa ya namna hiyo, uwanja huo ambao ulifunguliwa mwaka 1931 uliwahi kufungiwa na FIFA mwaka 2007 kutokana na wachezaji wa timu mgeni kuona Bolivia wanapata unfair advantage.
Bahati waliyokuwa wameipata Brazil ni kucheza katika uwanja huo wakiwa tayari wamefanikiwa kufuzu Kombe la dunia, tofauti na Argentina na Chile ambao waliingia katika uwanja huo wakiwa wanahitaji matokeo kitu ambacho walijikuta wanaondoka na kipigo.
VIDEO: Kitu Samatta kaongea kabla ya kucheza na Malawi kesho