Staa wa soka wa kimataifa wa Italia ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Inter Milan, AC Milan na Juventus vya kwao Italia Andrea Pirlo ametangaza kuwa atastaafu soka mwisho mwa mwaka 2017 akiwa na club ya New York City FC ya Marekani.
Andrea Pirlo mwenye umri wa miaka 38 ameweka wazi mpango wake wa kustaafu soka mwezi December 2017 mara tu mkataba wake utakapomalizika mwezi December, hiyo inatokana na nafsi yake kuona inatosha sasa ni zamu ya vijana wenye umri mdogo kupata nafasi.
“Kwa umri wangu sasa inatosha sio kwamba unaweza kucheza soka maisha yako yote hata ukiwa na umri wa miaka 50, nitafanya kitu kingine cha ziada, katika umri wa miaka 38 ni wakati sahihi wa kuachia nafasi za kucheza soka vijana wadogo sina hasira na nikiondoka nitapeana mikono na wachezaji wenzangu na kocha”>>> Pirlo
Pirlo hadi anastafu soka amefanikiwa kushinda mataji sita ya Ligi Kuu Italia maarufu kama Serie A, mataji mawili ya UEFA Champions League na kuisaidia timu yake ya taifa ya Italia kushinda Kombe la Dunia 2006, hata hivyo Pirlo amecheza mechi 15 kati ya 32 za New York City msimu huu.
ALL GOALS: Taifa Stars vs Malawi October 7 2017, Full Time 1-1