INAFAHAMIKA wazi kuwa wamiliki wa Kampuni, Ofisi ama kitu chochote ndio huwa na mamlaka mengi juu ya kila kitu; ndio huamua nini kifanyike na nani afanye, kitu gani kisifanywe na hakuna mtu ambaye anaweza kuhoji na mara nyingi ndio huamua nani afanya kazi na nani asifanye.
Sasa stori ya kushangaza ambayo imenifikia ambayo imechapishwa na mtandao maarufu wa The Guardian Jumatatu ya October 9, 2017 ni kwamba mambo yameenda kinyume baada ya mmiliki wa kampuni ya Weinstein Company, Harvey Weinstein kufutwa kazi na Bodi ya Wakurugenzi wake baada ya kuvuja taarifa kuwa alifanya unyanyasaji wa kijinsia.
Weinstein – ambaye ni producer maarufu wa Hollywood aki-produce filamu kama Pulp Fiction na Gangs of New York – aliwekwa kikaangoni baada ya kuvuja taarifa za udhalilishaji wa kingono ambayo yalifichuliwa wiki iliyopita na New York Times exposé. Bodi ilikaa Ijumaa na kupitisha maamuzi hayo lakini wakaenda mbali zaidi Jumapili, kumuondoa kwenye kampuni aliyoiasisi.
The Weinstein Company ni kampuni ya filamu ambayo Makao yake Makuu yapo New York City na waasisi wake ni Bob Weinstein na Harvey Weinstein ambapo waliianzisha mwaka 2005.
MOTO ARUSHA! Mwalimu kasimulia Wanafunzi zaidi ya 100 wanavyolala Msikitini
KITANZINI: Eneo la kihistoria lililotumiwa na WAKOLONI kuwanyonga WAHEHE
Agizo la Waziri Mwigulu “Tusitafute ugomvi na Serikali za Nchi hizi…”