Watu watatu akiwemo Meneja wa Benki, Khalid Mwinyi mwenye umri wa miaka 33 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za mauaji ya Mkurugenzi na Mwanzilishi-Mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, Wayne Lotter ambaye alikuwa na umri wa miaka 52.
Watuhumiwa wengine ni mfanyabiashara Rahma Almas maarufu baby mwenye miaka 37 na Mohammed Maganga mwenye umri wa miaka 61 ambaye ni mchimba makaburi.
Akiwasomea kosa lao Wakili wa Serikali, Adolf Mkini mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na kosa la mauaji ambapo wanadaiwa walitenda kosa hilo August 16, 2017 katika makutano ya barabara za Chole na Haike Selasie Kinondoni DSM, ambapo walimuua Lotter.
Baada ya kusomewa kosa hilo, Hakimu Mashauri alisema kosa hilo halidhaminiki na Mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo ameahirisha kesi hadi October 23, 2017.
MOTO ARUSHA! Mwalimu kasimulia Wanafunzi zaidi ya 100 wanavyolala Msikitini