Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) imepokea wataalamu 16 kutoka nchini Cuba kama moja ya mikakati yake ya kuboresha utoaji huduma za Afya nchini ikiwa ni pamoja na huduma ya kurekebisha muonekano wa macho ambayo yalipata hitilafu ya kiafya au kutokana na ajali.
Imeelezwa kuwa uwepo wa wataalamu hawa utapunguza wagonjwa kusafirishwa kwenye nje ya nchi kwa ajili ya matibabu lakini pia utapunguza mrundikano wa wagonjwa wanaosubiri kupatiwa huduma hospitalini.
Ulipitwa na hii? GOOD NEWS: “Jicho lililopata hitilafu kurudishiwa muonekano mzuri na kupendeza zaidi” – Muhimbili