Utafiti mpya uliofanywa na Chuo cha tiba ya miguu nchini Uingereza umeeleza kuwa tabia iliyoenea ya vijana hususani wanaume kuvaa viatu bila soksi imesababisha ongezeko maambukizi ya maradhi ya miguu yanayosababishwa na kuvu.
Mtaalamu Emma Stephenson anasema amekuwa akipokea wanaume wa kati ya miaka 18-25 walio na matatizo kwenye miguu yao ambayo yametokana na kutovalia soksi au kuvalia viatu visivyowatosha vizuri.
Imeelezwa kuwa kwa kawaida miguu hutoa kiasi cha jasho cha 0.28 kila siku na hivyo unyevumwingi ya joto hilo husababisha muwasho na michubuko ambayo huleta magonjwa ya ngozi ya miguu.
Ulipitwa na hii? Kwanini kwenye kesi za uchochezi wanapimwa mkojo? Mkemia Mkuu kajibu