Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, leo October 10, 2017 ametangaza kutoshiriki kwenye uchaguzi mkuu ambao uliamriwa na mahakama kurudiwa October 26 mwaka huu.
Baada ya Raila Odinga kujiondoa katika kugombea kiti cha Urais katika uchaguzi Mkuu wa marudio uliyopangwa kufanyika October 26, mpinzani wake Uhuru Kenyatta ameongea mawazo yake baada ya Raila kujitoa.
“Sasa umesema umejitoa baada ya kutupeleka kutupeleka sasa ndio unasema umejitoa zaidi ya shilingi Bilioni 12 ambazo zinatumika kufanya uchaguzi ambazo zingejenga hospitali barabara unasema umejitoa hakuna mahali ambapo katiba imesema kuwa lazima Raila Omolo Odinga ashiriki uchaguzi”>>>Uhuru Kenyatta
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga Septmber 1 2017 alitengua matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Kenya kwa madai kuwa, haukuwa uchaguzi wa huru na haki, hivyo kwa mujibu wa katiba ya Kenya uchaguzi uliamuriwa kufanyika ndani ya siku 60.
Uhuru Kenyatta baada ya kusikia mpinzani wake Raila Odinga amejitoa kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu October 26 2017 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/F54QANkrwQ
— AyoTV (@AyoTV) October 10, 2017
Ulipitwa na hii? Baraza Jipya la Mawaziri laanza kazi rasmi