Leo October 11, 2017 aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki amekabidhi Ofisi kwa Waziri mteule wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapt.(Mstaafu) George Mkuchika.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Waziri Kairuki ametaja mambo matano ambayo yalikuwa changamoto kwenye wizara hiyo.
1. Changamoto ya kuunganisha kazi zilizokuwa zikifanywa na mawaziri watatu na kufanywa na wizara moja.
2. Zoezi la uhakiki
3. Changamoto ya maafisa wengine kutokuwa waaminifu kwenye zoezi la uhakiki
4. Changamoto ya maslahi kwa watumishi wa umma “Tuna idado kubwa ya watumishi lakini ukiangalia mapato ya Serikali kwa ujumla wake, kama serikali ungependa uongeze kwa kiasi kikubwa kulingana na gharama za maisha zinavyoongezeka” – Waziri Kairuki
5. Changamoto nyingine nyingine ni kurejesha nidhamu kwa watumishi wa umma “wengi walizoea kufanya kazi kwa mazoea”-Waziri Kairuki
“Hatutamvumilia yeyote atakayechelewesha ujenzi huu wa reli ya Standard Gauge” – RAHCO