Wakati baadhi ya vyama vya siasa vikikosoa hatua ya Rais John Magufuli kumteua Katibu mpya wa Bunge, Mwanasheria na Wakili wa kujitegemea amejitokeza kumkingia kifua Rais.
Katibu mpya wa Bunge Steven Kigaigai aliteuliwa October 7, 2017 na Rais wakati anafanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Wakili Leonard Manyama amesema Rais Magufuli hajavunja Katiba katika uteuzi wake akisema anapewa mamlaka ya kumteua Katibu kwa mujibu wa Ibara ya 87(1) ya Katiba ya Tanzania.
>>>”Mamlaka ya kuteuliwa kwa Katibu anayo Rais, ambapo kwa mujibu wa Ibara hiyo anapaswa kuteuwa mtu miongoni mwa watu wenye madaraka ya juu, nafasi na uzoefu.”
Aidha, Wakili Manyama amesema kuwa Ibara hiyo inajitosheleza na haitegemei Sheria yoyote ya kuifafanua na ameliomba Bunge lipitie upya baadhi ya Sheria ili kuondokana na utata kama wa namna hiyo.
>>>”Mathalani, kifungu cha Katiba cha 7(3) cha Sheria ya Utawala wa Bunge kinampa mipaka Rais juu ya uteuzi wa Katibu – kwamba ateuwe watu watatu ambao watachaguliwa, lakini katika Katiba anapewa mamlaka ya moja kwa moja.”
Manyama amesema kuwa katika Katiba yapo maeneo ambayo utekelezaji wake unakuwa wa moja kwa moja kwa baadhi ya Ibara ambazo hazihitaji Sheria yotote.
Raisi Magufuli kafanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri
Rais Magufuli alivyoutaja mshahara wake kwa mara nyingine