Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imekwama kusikiliza ushahidi wa kesi ya uhujumu uchumi wa Meno ya Tembo yenye thamani ya Tsh. Bilioni 13 inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan ‘Malkia wa Meno ya Tembo’ kwa sababu Shahidi hajatokea Mahakamani.
Wakili wa Serikali, Paul Kadushi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa kesi hiyo ilipaswa kuendelea kusikilizwa leo October 17, 2017 na kwamba walimuita shahidi mmoja kwa ajili ya kutoa ushahidi lakini amepata dharura na hakuweza kufika.
Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko alidai kuwa alitegemea upande wa Mashtaka ungeandaa Mashahidi wawili ama watatu ili mmoja akipata udhuru wengine waendelee.
Kutokana na hatua hiyo, Nkoko ametaka waandaliwe Mashahidi watatu ili hali kama hiyo isijirudieambapo baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi October 18, 2017 ambapo itasikilizwa siku tatu mfululizo.
Mbali ya Glan, Washtakiwa wengine ni Salvius Matembo, Philemon Manase ambapo wanadaiwa kuwa kati ya January na May 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali.
Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 na thamani ya Tsh Bilioni 5.4 bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyama Pori.
BREAKING NEWS: TAKUKURU yamuonya Joshua Nassari “tunatoa onyo jingine”
UNATAKA KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI? Breaking NEWS, Za Mastaa, Siasa, Michezo na nyingine…. fanya jambo moja tu rahisi… BONYEZA PAGE ZIFUATAZO ili nikutumie kila kitu kiganjani mwako >>> INSTAGRAM <<<< FACEBOOK >>>> TWITTER >>> APP MPYA YA MILLARD AYO pia bonyeza SUBSCRIBE HAPA >>> YOUTUBE