“Acheni kufanya biashara za kuuza vitumbua ili upeleke mtoto wako shule…. fanya biashara ya vitumbua kwasababu unataka baada ya muda uuze vitumbua nchi nzima, nataka uwaze kama Azam” Ruge Mutahaba ameanza kwa kuongea maneno hayo.
Fursa 2017 ilikuwa zamu ya Mbeya October 17, 2017 ambapo Watu wa Mbeya walipata darasa la bure kabisa kuhusu namna bora ya kujisogeza kimaisha na kuongeza thamani.
Ruge ambae pia ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge alisema “tuachane na dhana ya kutafuta mkate bali tutengeneze dhana za kukua na kuwa Wakubwa kibiashara”
“Kinachotusumbua ni kitu kimoja tu, matumizi yetu hayalingani na mapato yetu… tuchukulie kila mtu hapa mapato yake kwa mwezi ni shilingi laki 5 lakini kihalali matumizi yetu wote ni laki 8 na kwenda juu, hiyo laki 3 iliyozidi ndio inatupa shida wote”
“Hiyo tofauti ya laki 3 ndio inatuendesha… hapo lazima uibe kama utapiga dili kazini ni kuhangaikia ile laki tatu, tunalaumiwa tu na Waheshimiwa hawa… sio halali na sio sawa lakini tunafanya” – Ruge
Si ndio sisi Watanzania ambao hatuwezi kuacha kutoa michango ya harusi na kitchen party ambayo inaonekana ni lazima wakati sio lazima? tumeshazoea kujifikiria watanielewaje nisipotoa mchango…. ukweli ni kwamba ni lazima tupunguza matumizi kwenye maisha yetu ya kila siku
Mtazame Ruge Mutahaba akiongea zaidi kwenye hii video hapa chini