Moja ya habari kubwa za Tanzania leo October 30 2017 ni kujiuzulu kwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu ambae pia ametangaza kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Baada ya kauli hiyo AzamTV imemuhoji Katibu Mkuu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole ambae amesema “Ni jambo la kawaida kabisa mtu ambae ameondoka anazo haki zote, wameondoka Wazito kwenye chama hiki na chama kimebaki kimoja kwahiyo huyu sio sehemu ya wazito, ni Mwananchi ambae ana haki ya kufanya hivyo“
“Kwenye chama cha Mapinduzi kila kipindi ambacho tumekua tukifanya mageuzi makubwa ambayo yanatoa tafsiri pana ya kifikra na kuonyesha mwelekeo mpya, watu wengi huputika… nina uhakika wako kadhaa ambao wanashindwa kwenda na mwendokasi huu sasa kabla shoka halijawekwa shinani unakimbia mapema” – Polepole
CHADEMA kwa upande wake kimesema “Chama cha siasa ni watu na hakuna chama cha siasa ambacho kitasema hatutaki watu, tunampongeza sana kwa uamuzi wake huo na ni uamuzi wa kizalendo, muda muafaka ukifika tutampokea”
ULIPITWA? Tazama hapa chini Lazaro Nyalandu akitangaza kujiuzulu, bonyeza play hapa chini
VIDEO: Mama alieangua kilio mbele ya Rais Magufuli Mwanza, bonyeza play hapa chini kumtazama na maamuzi ya Rais Magufuli