Mtandao wa Instagram ni moja kati ya mitandao ya kijamii inayopendwa na kutumiwa na watu wengi sana duniani. Ina watumiaji zaidi ya milioni 250 duniani kote na kumekuwa na mabadiliko mbalimbali ambayo yamefanyika kwenye mtandao huu tangu umeanzishwa. Vifuatavyo ni vitu 5 ambavyo yawezekana huvifahamu kuhusu mtandao huu wa Instagram
Instagram ni nini?
Ni mtandao ambao ni kwa ajili ya kushare picha na video za matukio yao mbalimbali. Hapo awali wakati Instagram inaanzishwa kilichofanya mtandao huu kupenda ilikuwa ni idadi ya filter ambazo zinawezesha mtumiaji kuhariri picha zake kwa jinsi anavyopenda. Pia Instagram ilikua inaruhusu kupost picha za kipimo au umbo la mraba tu yaani square.
Hata hivyo mabadiliko yalifanyika ilipofika August 2015 kwenye size za picha za kuweka kwenye mtandao huo ambapo watumiaji waliruhusiwa kuweka picha za maumbo yoyote bila tena kulimitiwa na umbo la picha za square.
Watu gani haswa wanatumia Instagram?
Inaelezwa kuwa mtandao wa Instagram ndio unaotumiwa na watu wa matabaka yote ya jamii katika maeneo mbalimbali duniani. Watafiti wa masoko wameeleza kuwa 90% ya watumiaji wote wako chini ya umri wa miaka 35 na kati yao 68% ni wanawake wakati 70% kati ya watumiaji wote duniani hupitia akaunti zao angalau mara moja kwa siku.
Inaelezwa pia kuwa mtu maarufu duniani ambaye anapicha za selfie nyingi kwenye akaunti yake ya Instagram ni mwanamitindo wa Marekani Kylie Jenner ambaye ni mdogo wa Kim Kardashian ambaye ana selfies zaidi ya 450, huku celebrity mwenye followers wengi zaidi Instagram ni mwanamziki Selena Gomez mwenye followers milioni 128.
Instagram inatumiwa wapi?
Kwa watumiaji wa simu za mkononi, watumiaji wa Instagram ni wengi sana kuliko wanaotumia Twitter kwenye simu zao. Japokuwa ilitengenezwa na kuzinduliwa nchini Marekani, ni 40% tu ya watumiaji wote wa mtandao wa Instagram wanaishi nchini humo, na nchi za Brazil na Japan ndizo zinazoingia kwenye top 3 ya nchi zenye idadi kubwa ya wanaotumia mtandao huo baada ya Marekani.
Instagram ilitengenezwa lini?
Mtandao huu ulitengenezwa mwaka 2010 na Kevin Systrom and Mike Krieger. Ilizinduliwa rasmi kama programu ya Kampuni ya Apple April 2010. Na baada tu ya kuzinduliwa ilipata watumiaji milioni 1 ndani ya mwezi mmoja na kutokana na hili, Kampuni ya Facebook iliamua kuinunua programu hii April 2012.
Kampuni ya Facebook iliinunua App hiyo ya Instagram kwa Dola za Marekani bilioni 1 ambayo ni sawa na takriban Tsh trilioni 2.4. Wakati Instagram inanunuliwa na facebook, ilikua na wafanyakazi 13 tu na ilipofika April 2012 Instagram ilianza kupatikana katika simu za Android jambo lililoelezwa kuwa lilikuwa la mafanikio makubwa sana.
Baada tu ya Instagram kuingizwa system ya simu za Android takriban watu milioni 1 walidownload program hii na kuanza kuitumia ndani ya masaa 12. Ilipofika June 2013 mabadiliko kadhaa yalifanywa kwenye mtandao huu ambapo watumiaji waliweza kuanza kupost video fupi kwenye akaunti zao zisizozidi sekunde 15. Mabadiliko haya yalipelekea kupostiwa video takribani milioni 5 ndani ya saa 24.
Kwanini Instagram inafahamika na kutumiwa na watu wengi zaidi duniani?
Instagram inafahamika sana kwasababu kwanza ni mtandao ambao unapatikana bila malipo yoyote tofauti na baadhi mitandao ya kijamii lakini pia mtandao huu umetajwa kuwa umeongeza ubunifu wa watu ambao wanajitahidi kupost picha na video nzuri kwa kuzihariri kabla ya kuzipost, jambo ambalo limeongeza watu kufahamiana zaidi.
Sababu nyingine ni kwamba Instagram inaruhusu watumiaji wake kupiga na kupost picha aina ya selfie, ambazo ni picha za mtu aliyejipiga picha mwenyewe. Inaelezwa kuwa kuna selfies zaidi ya milioni 60 zilizopostiwa kwenye mtandao huu ambazo zina hashtag ya selfie. Inaelezwa pia kuwa hashtag zinazotumiwa zaidi kwenye mtandao huu ni love, me, beautiful na hashtag tbt. Na 83% ya post zote za Instagram zinaelezwa kuwa na hashtag.
Ulipitwa na hii? MAMBO 8 YA VITUKO NA KUSISIMUA KWENYE HARUSI YA JOTI