Wanasema tenda wema nenda zako…. Mzee Masele wa Mwanza zaidi ya miaka 20 iliyopita hakujua kwamba ameitoa shilingi Elfu 10 yake kumsaidia Rais mtarajiwa wa Tanzania.
Wakati huo President Magufuli alikua kijana na Mzee Masele ndio mtu pekee aliemchangia Dr. Magufuli shilingi elfu 10 kwa ajili ya fomu ya kugombea Ubunge japokua Mzee huyo alikua ana wasiwasi kama Dr. Magufuli angeshinda Ubunge maana hakuwa na pesa.
Sasa leo wakati President Magufuli yuko kwenye siku yake ya pili ya ziara ya kikazi Mwanza alikua na Mzee Masele kwenye eneo la tukio, akakumbuka hata maneno ambayo Mzee Masele alimwambia baada ya kumchangia shilingi elfu 10.
“Utaweza kwenda kuomba Ubunge kijana na hela tunajua huna? nikasema Mungu atanisaidia na yeye akasema basi tunakuombea…. na nilipoenda nikashinda bila kutumia pesa yoyote” – JPM
Kutazama video nzima ya kilichoendelea na pesa alizozitoa Rais Magufuli livelive bonyeza play kwenye hii video hapa chini kujionea…..
VIDEO: Alichoagiza Rais Magufuli baada ya Mwanamke kuangua kilio mbele yake Mwanza, bonyeza play hapa chini kutazama