Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesogeza mbele hukumu ya kesi ya kutoa taarifa ya uongo kupitia mtandao wa Facebook, inayomkabili Bob Chacha Wangwe, November 15, 2017.
Bob ambaye ni Mwanaharakati ni mtoto wa marehemu Chacha Wangwe, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime, mkoani Mara na Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara.
Hukumu hiyo ilitarajiwa kusomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambapo amesema ameshamaliza kuiandaa hukumu hiyo lakini anaona ni vyema akaisoma tarehe ijayo.
“Hukumu nimeshamaliza kuiandaa kila kitu, hivyo nitaisoma November 15,2017,”.
Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi 6, upande wa utetezi ukiwa na shahidi mmoja ambaye ni mshtakiwa mwenyewe.
Awali katika ushahidi wake, Bob amedai kuwa yeye hakuandika maneno ya upotoshaji wala hajawahi kufanya hivyo.
“Mimi nilitoa maoni yangu kuhusu uchaguzi wa Zanzibar na kasoro zake za kidemokrasia kama Watanzania wengine na waangalizi wa uchaguzi huo walivyofanya,”.
Katika kesi hiyo namba 167, Chacha Wange anatuhumiwa kwa kosa la kuchapisha taarifa za kupotosha katika ukurasa wake wa mtandao wa Facebook.
Ulipitwa na hii? Kesi ya Lulu leo na Baba yake alivyokimbizana na Waandishi