Ni kutoka Bungeni Dodoma leo November 9 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisimama Bungeni Dodoma kujibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Wabunge na moja ya maswali aliyoyajibu ni lililoulizwa na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe.
Mbowe alianza kwa kusema “tukio la Mbunge Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi limezua hofu kubwa sio tu kwa taifa na nina uhakika taharuki hiyo imeharibu sura ya taifa, heshima tuliyokua nayo kama taifa na hatujaona kama Serikali inachukua hatua zozote kujaribu kufanya jambo hili lisiendelee kuharibu ‘image’ ya taifa”
“Aidha Mh. Waziri Mkuu utakumbuka hapo nyuma vimetokea vifo vya kisiasa, alifariki Mwenyekiti wetu wa mkoa wa Geita, Msaidizi wangu Ben Saanane, kushambuliwa kwa Tundu Lissu pia tumeomba Serikali iruhusu vyombo vya kimataifa vya uchunguzi bado serikali imeonekana ina kigugumizi” – Mbowe
MAJIBU YA WAZIRI MKUU:
“Kwanza nataka nieleze kwamba amani yetu, utulivu ndani ya nchi ni jambo ambalo Watanzania wote ni lazima tushikamane, tushirikiane katika kulidumisha…. yako matukio yanajitokeza, Mh. Mbowe umezungumzia upande wa siasa lakini matukio haya yapo kwa ujumla wake nchini kwenye maeneo kadhaa kwa ngazi ya familia na maeneo mbalimbali”
“Wako wenzetu ambao hawana nia njema nchini wanajitokeza katika kutenda matendo hayo… hata hili unalolisema la Mh. Tundu Lissu sio Mh. Tundu Lissu pekee ingawa hatupendi mambo kama haya yatokee lakini pia tumepoteza Watanzania wengi hata unakumbuka Mkuranga, Kibiti na Rufiji, hata siku za karibuni kamanda wetu wa JWTZ alipigwa risasi pia kwahiyo tuyazungumze haya kwa ujumla wake”
“Nataka nikuhakikishie kwamba vyombo vyetu vya dola vinaendelea kufanya uchunguzi wa haya, uchunguzi huu hauwezi kuwa leoleo ukapata ufumbuzi kwasababu wanaotenda matendo haya wanatumia mbinu nyingi za kujificha” – WAZIRI MKUU MAJALIWA
Bonyeza play kwenye hii video hapa chini kutazama mwanzo mwisho alichoeleza Waziri Mkuu..
UNAZITAKA BREAKING NEWS FASTAFASTA? Jiunge na Reporter wako Millard Ayo kwa kubonyeza kifuatacho SUBSCRIBE >>> YOUTUBE , APP YA MILLARD AYO, FACEBOOK , INSTAGRAM