Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Hispania katika club ya Tenerife B, juzi ziliripotiwa taarifa za hatari kuhusiana na jeraha lake la goti na alikuwa na hatari ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha msimu kilichosalia.
Good News iliyotangazwa leo kutoka Hispania ni kuwa Farid Musa akizungumza na mtandao wa habari za michezo wa shaffihdauda.co.tz ameeleza kuwa uchunguzi wa kina umefanywa na jopo la madaktari na imegundulika kuwa jeraha lake la goti halihitaji upasuaji kama ilivyokuwa inadhaniwa awali.
“Daktari amesema sijaumia sana kiasi cha kufanyiwa upasuaji, ni mishipa tu ilipishana, kwa hiyo amenipa wiki tatu za kufanya mazoezi chini ya uangalizi wa physiotherapist wa klabu, baada ya hapo naweza kuanza mazoezi ya kawaida”-Farid Musa
Farid Musa kuikosa Taifa Stars vs Benin kama Samatta