Utafiti mpya uliofanywa huko Uingereza umeonyesha kuwa saratani au uvimbe kwenye matiti unaweza kurudi miaka 15 baada ya kutibiwa na kupona kabisa.
Taarifa iliyotolewa na BBC imeeleza kuwa Wanawake ambao walikua na uvimbe mkubwa na saratani kabla na wakati wa kutibiwa wako katika hatari ya 40% ya ugonjwa huo kurudi siku za mbeleni.
Mtafiti Mkuu wa Utafiti huo kutoka Chuo Kikuu cha Oxford Dr Hongchao Pan ameeleza kuwa kwakuwa kwa sasa tiba ya saratani ya matiti ni ile ya miaka mitano, utafiti unaonesha kuwa kuna umuhimu wa tiba hii kufanywa kwa miaka 10 ili isaidie kupunguza hatari ya saratani hiyo kujirudia.
ULIPITWA? MWANAMKE MWENYE NDEVU ALIVYOOMBWA NDEVU ZAKE ZIMTAJIRISHE MTU KISHIRIKINA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA