Inawezekana wewe ni mmoja kati ya wengi ambao hawajawahi kusikia kuwa kidonda ambacho kimepatikana nyakati za mchana huwa kinapona haraka kuliko kile kilichopatikana usiku.
Utafiti mpya uliofanywa nchini Uingereza kwenye Maabara ya Baiolojia nchini humo ijulikanayo kama MRC Laboratory of Molecular Biology umegundua kuwa vidonda vinavyopatikana mchana hupona haraka kuliko vile vya siku kutokana na uwezo wa seli aina ya fibroblasts ambazo hufanya kazi vizuri wakati wa mchana.
Seli za fibroblasts zinaelezwa kuwa ndio vijibizi vya kwanza kwenye mwili wa binadamu ambazo huenda moja kwa moja tena wakati huohuo kilipotokea kidonda na kuanza kukifunga. Seli hizi zinaelezwa kuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi wakati wa mchana na hupoteza uwezo wake wakati wa usiku.
Timu ya wachunguzi wa utafiti huu walifanya uchunguzi kwa kuangalia vidonda 118 vya wagonjwa waliopata makovu ya kuungua moto ambapo waligundua kuwa wagonjwa walioungua nyakati za usiku vidonda vyao vilichukua hadi siku 28 kupona wakati walioungua mchana iliwachukua siku 17 hadi kupona kabisa.
“Tumeanza kuwatoa wapangaji wa ofisi na biashara, watu binafsi wajiandae” Shadrack Nkelebe