Shirika la utangazaji la Uingereza BBC baada ya kukaa na kupitia vigezo vyao limetangaza list ya majina matano ya wachezaji wa Afrika watakaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika wa BBC kwa mwaka 2017.
BBC wametangaza majina ya wachezaji watano ambao kwa mwaka 2017 ndio watawania tuzo ya mchezaji bora Afrika wa BCC, waliyotajwa katika kuwania tuzo hiyo ni Sadio Mane wa Senegal anayecheza Liverpool, Mohamed Salah wa Misri anayecheza Liverpool.
Wengine waliyotajwa katika list hiyo ni pamoja na Victor Moses wa Nigeria anayeichezea Chelsea, Piere Emerick Aubameyang wa Gabon anayecheza Borussia Dortmund ya Ujerumani na mwisho alikuwa ni Naby Keita wa Guinea anayecheza soka RB Leipzig ya Ujerumani.
Kura zinaendelea kupigwa lakini list au mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa BBC kwa mwaka 2017 atatangazwa Jumatatu ya December 11 2017 na itaoneshwa live na BBC World TV na BBC World Service Radio.
Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji