Baraza la mitihani la Taifa NECTA kupitia kwa katibu mtendaji wake Dr Charles Msonde amezungumzia kuhusu upimaji wa kitaifa kidato cha pili utafanyika Tanzania bara kuanzia Jumatatu November 13 hadi November 24 2017 kwa za sekondari 4705.
“Tungependa kuwaarifu watanzania wafahamu kuwa upimaji wa kitaifa wa kitado cha pili kwa mwaka 2017 utafanyika Tanzania bara kuanzia November 13 hadi November 24 2017 lakini tarehe 22 na 23 mwezi November utafanyika pia upimaji wa kitaifa wa darasa la nne”- Dr Msonde
“Dhana ya upimaji ya kitaifa utofautiana na ile ya upimaji wa mitihani ya taifa kwa kuwa upimaji wa kitaifa hufanywa katikati ya mafunzo wakati mitihani ya taifa hufanywa mwishoni mwa mafunzo katika upimaji wa kidato cha pili jumla ya wanafunzi 521855 ndio wamesajiliwa kufanya upimaji huo”-Dr Msonde
“Kati ya hao waliosajiliwa wavulana wapo 251570 sawa na asilimia 48.21 na wasichana wapo 270285 sawa na asilimia 51.79 katika upimaji huo wa kidato cha pili pia tutakuwa na watahiniwa 56 wasioona na watahiniwa 330 wenye uono hafifu ambao maandishi yao yanakuzwa ili waweze kuona”- Dr Msonde
Ayo TV MAGAZETI: Nyalandu aanza kazi CHADEMA, Maajabu tajiri aliyetaka kununua hekalu za Lugumi