Shirikisho la soka Ulaya UEFA Ijumaa ya November 10 2017 lilitangaza kumuadhibu beki wa kimataifa wa Ufaransa anaeichezea Olympique Marseilleya Patrice Evra kwa kosa la kumpiga Shabiki wao wakiwa Ureno kwenye mchezo wa Europa League.
UEFA walitangaza kumfungia Evra kucheza mashindano yoyote ya UEFA hadi mwezi June 2018 kwa kosa la kumpiga teke shabiki, adhabu ambayo imepelekea Marseille wavunje mkataba na Evra lakini leo Evra amepost video Instagram ikimuonesha akivuta gari huko Dubai.
“Wakati mwingine maisha unaweza kufikiri ni magumu sana lakini siku zote inatakiwa uishi na kutabasamu, naapa kwa Mungu nitarudi nikiwa imara zaidi ya ambavyo nimewahi kuwa usikubali kuwa mzembe nataka kuwa bora kuliko nilivyokuwa awali” – Patrice Evra
Beki wa Marseille Patrice Evra baada ya kufungiwa na UEFA hadi mwezi June 2018 kucheza mashindano yoyote ya UEFA kwa kosa la kumpiga shabiki #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/28UmJnv6C7
— AyoTV (@AyoTV) November 13, 2017
Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji