Usiku wa November 13 2017 ndoto ya kushiriki fainali za Kombe la dunia 2018 nchini Urusi kwa timu ya taifa ya Italia ilizimwa na timu ya taifa ya Sweden katika ardhi ya Italia, hiyo ni baada ya Sweden kuilazimisha Italia sare tasa na kuiondoa kwa ushindi wa jumla ya goli 1-0 iliyoupata Sweden katika mchezo wa kwanza nyumbani.
Baada ya kutolewa jana katika kufuzu Kombe la Dunia Italia ndio wanakuwa wameshindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza toka 1958 ambapo walikuwa wakifanikiwa kushiriki mfululizo, umiliki wa mpira kwa asimilia 76 kwa 24 haukuweza kuisaidia Italia ikiwa katika uwanja wao wa San Siro.
Miongoni mwa vitu vilivyowashangaza wengi katika game hiyo muhimu ambayo Italia ikuwa inahitaji ushindi ni maamuzi ya kocha wa Italia Giampiero Ventura kumuweka benchi Lorenzo Insigne wa Napoli ambaye msimu huu amefunga magoli sita na kutoa pasi tano za magoli, hivyo baadhi wanaamini angeweza kumchezesha pengine angeweza kusaidi Italia katika game hiyo ambayo ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yoyote.
Baada ya Italia kushindwa kufuzu kushiriki michuano hiyo kwa mwaka 2018 nahodha wao Gianluigi Buffon ambaye amecheza fainali sita za Kombe la dunia, ametangaza kustaafu kucheza soka la kimataifa, maamuzi hayo yanakuja baada ya kuichezea Italia kwa jumla ya game 175 akiruhusu kufungwa magoli 124 lakini amefanikiwa kucheza game 64 bila kuruhusu goli.
Kiungo mkabaji wa Roma Daniele De Rossi alikuwa sehemu ya kikosi cha Italia kilichokuwa kinapambania nafasi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Sweden alinaswa na Camera akigoma kwenda kufanya warm ili aingie kwa kigezo kimoja tu baada ya kuambiwa afanye warm up akasema “ Kwa nini niingie hatuhitaji droo game hii sisi tunahitaji ushindi”
Taarifa rasmi kutoka Ubelgiji, Samatta atafanyiwa upasuaji