Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Bob Chacha Wangwe mtoto wa Mbunge wa zamani wa Kiongozi wa CHADEMA kufungwa jela mwaka mmoja na nusu au kulipa faini ya milioni 5 ikiwa ni baada ya kupatikana na hatia ya kusambaza habari za uongo kupitia mtandao wake wa Facebook.
Baada ya hukumu hiyo Bob amelipa faini na kuachiwa huru lakini alipotoka nje ya Mahakama akasema hajakubali bado, “Kwanza kabisa sijaridhika na uamuzi ambao umetolewa na Mahakama, Hakimu hajasema ni kwanini au ule ujumbe wangu niliopost ulikua na uchochezi au haukuwa na uchochezi”
“Nitakata rufaa kwenda Mahakama kuu ili tuwe huru sababu swala lolote la kutoa maoni sio swala la mjadala, ni swala ambalo lipo kikatiba na ni haki yetu ya msingi” – BOB CHACHA
Mtazame zaidi akiongea kwenye hii video hapa chini Bob akiongea leo
DR. LUIS SHIKA ASEMA “MIMI SIO MBAMBAISHAJI” AONYESHA KAMPUNI YAKE
VIDEO YA LULU KWENYE GARI LA POLISI AKIPELEKWA GEREZANI…. BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA