Siku hadi siku bara la Afrika linaendelea kuisogelea Teknolojia na kufanya vitu ambavyo tumezoea kuviona ni vya kawaida kwa nchi za wenzetu ambapo sasa kuna magari yanatengenezwa kwenye nchi za Afrika.
KENYA
Nchi ya kwanza ni Kenya ambapo kampuni ya Mobius Motors ambayo ilianzishwa na Mwekezaji Muingereza mwaka 2009 inatarajia kuanza kuuza Mobius II mwaka 2018 na tayari wameshaanza kupokea oda, picha zake ndio hizi hapa chini.
Bei ya Mobius inaanzia Milioni 27 za Kitanzania.
UGANDA
Nchi ya pili ni Uganda ambapo magari yanatengenezwa na KIIRA MOTORS ambayo pia mpango wao ni kuleta aina mpya ya gari ya kutembelea mwaka 2018 tofauti na mwanzoni walivyoanza kwa kutengeneza Mabasi.
Inaripotiwa kwamba Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewekeza Dola za Kimarekani MILIONI 43.5
NIGERIA
Nigeria ni nchi ya tatu kwenye hii orodha ya nchi 5, wenyewe wanayo hii Innoson Motors iliyoanzishwa na Mnigeria Innocent Chukwuma ikiwa ni kampuni ambayo iliingiza sokoni magari kadhaa ya kutembelea mwaka 2014.
TUNISIA:
Namba 4 ni Tunisia ambao wana WallysCAR kampuni iliyoanzishwa mwaka 2007, ni gari ambalo lina siti mbili na linabeba injini ya Peugeot ambapo kwa mwaka inaingiza sokoni magari yasiyopungua 600.
GHANA:
Kampuni ya Kantanka inatambulika kama kampuni ya kwanza kutengeneza magari yenyewe Ghana, ni magari ambayo bei yake inaanzia milioni zisizopungua 40 za Kitanzania ambapo Jeshi la Polisi ni miongoni mwa Wateja wao wakubwa.
Tanzania imewahi kuingia kwenye headlines za kutengeneza magari yake ambayo yalipewa jina la NYUMBU yakitengenezwa na kampuni ya MZINGA ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania lakini ni muda sasa hatujasikia kutoka Nyumbu, millardayo.com itafatilia zaidi kujua.
EXCLUSIVE VIDEO: MILIONEA MTANZANIA SUMRY HATAKI TENA KUSIKIA BIASHARA YA MABASI, KATUONYESHA ALIKOJICHIMBIA… MTAZAME KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
EXCLUSIVE VIDEO: HOTELI ALIYOIJENGA MR. II SUGU MBEYA… BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUITAZAMA