Jiji la Dar lina vitu vingi sana vya kuvutia na vingine vinavyochukiza,kwa haraka haraka endapo ukimuuliza mtu anayeishi Dar kitu gani anatamani kiondolewe kwa haraka pengine anaweza kupa kipaumbele cha foleni ndiyo kianze kushughulikiwa.
Si kwamba hakuna kero nyingine hapana,zipo na nyingi tu lakini hii ni miongoni mwa zile zinazowatesa wakazi wengi wa jiji hili kuna kipindi inakulazimu kutumia zaidi ya masaa mawili kwa sehemu ambayo pengine bila foleni ungetumia dakika 10 au 15 kufika.
Serikali iliamua kurahisisha usafiri wa Posta-Ubungo kwa kuweka reli ya kati ambayo inafanya safari hizo asubuhi na jioni inaonekana kama kupunguza japo si sana,kwa sasa wananchi wa Dar wanasubiri ujio wa mabus yaendayo kasi ambayo yapo kwenye mpango wa serikali na yanategemewa kuanza hivi karibuni.
Ukubwa wa foleni hizi hutegemea na muda kama una haraka ya kuwahi sehemu sa 2 asubuhi na unakoishi ni mbali pengine unalazimika kuamka hata saa 10 alfajiri,hivi ndivyo foleni ya Jiji la Dar inavyokuwa.