Wanawake wajawazito wameshauriwa kulala kwa upande badala ya kulala chali katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kupunguza hatari ya kujifungua watoto waliofariki tumboni.
Inaelezwa kuwa wajawazito wengi hupendelea kulala kwa mgongo jambo ambalo wataalamu wameeleza lina madhara makubwa sana kwa watoto hata kuweza kusababisha kifo.
Utafiti huu uliofanywa nchini Uingereza umeonesha kuwa takriban mimba 225 nchini humo huharibika na kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka huokolewa kwa wajawazito ambao hulala kwa kutumia upande wa kulia ama kushoto.
Ulipitwa na hii? SUMATRA: Marufuku ya kutoongelea siasa kwenye Mabasi TANZANIA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza yafuatayo Uchaguzi wa Udiwani