Dr. Shika hajawahi kuwa Msanii au kufanya kazi yoyote ya umaarufu kwenye maisha yake lakini jina lake liliibuka na kuwa kubwa ndani ya siku moja Tanzania na hapo ndio vichwa vya habari kuhusu yeye vikafata mfululizo.
Ni baada ya kuingia kwenye Mnada wa nyumba za Mabilioni na kujinadi kununua nyumba za Bilioni 2 huku akiwa hana senti 5 mfukoni, ikafanya watu wacheke na wengine kudharau wakiamini hakuwa sawa kichwani mpaka pale alipohojiwa na kueleza historia yake ndipo watu wakarudi kutamani kuyafuta maneno yao.
Leo hii Dr. Shika ameweza kupata pesa kutokana tu na umaarufu huo wa siku mbili ambapo amepata dili la Tangazo la Kampuni ya SOKA BET inayodili na michezo ya kubashiri.
Boss wa SOKA BET Franco Luinda amehojiwa na AyoTV na millardayo.com na kusema yafuatayo >>> “Sikuwahi kumfahamu wala sikutarajia kumfahamu Dr. Shika lakini nilimfahamu kupitia ule mnada wa Lugumi baada ya kuona video yake ina-trend sana Youtube“
“Tuliona tukimpata huyu Mzee na kufanya nae tangazo akiwa bado “hot” inaweza kutuletea Wateja wengi kwenye biashara yetu, kidogo ilikua mtihani kumpata na kumshawishi… nilimtafuta kwa muda wa kama siku 3 mpaka nikataka kukata tamaa lakini baadae nikampata ndio tukafanya hilo tangazo“
MTAZAME ZAIDI LUINDA AKIONGEA YOTE KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
VIDEO: DR. SHIKA ASEMA “MIMI SIO MBABAISHAJI” AONYESHA KAMPUNI YAKE… MTAZAME KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
BALOZI WA TANZANIA URUSI ASIMULIA WALIVYOMSAFIRISHA DR. LUIS SHIKA KUTOKA URUSI, BONYEZA HAPA CHINI KUMTAZAMA