Tunae Kamanda wa Polisi kwenye Mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah anaethibitisha kwamba tarehe 10 November 2017 ndio Polisi walipata taarifa rasmi kuhusu kifo cha utatanishi cha Mtoto ambae ni Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Scolastica iliyopo Himo Moshi Kilimanjaro.
Kamanda Issah ameendelea kwa kusema “Tulifanya mahojiano tukianzia na Mmiliki wa Shule, Walinzi na Majirani na baadhi ya Wanafunzi, katika mahojiano hayo kuna baadhi ya watu tuliwazuia ili kuendelea na uchunguzi”
“Tukishirikiana na Familia ya mtoto ambae alipotea ilikuja na plan B ambayo ilitusaidia na walisema mtoto wao tayari ameshafariki na moja kwa moja wanahusisha kifo hicho na Mmiliki wa hiyo shule” – Kamanda Issah
Makundi ambae ni Baba Mdogo wa Marehemu amesema “Tulipata taarifa ya mtoto kupotea tarehe 7 japo hatukua tunajua alipotea lini, tulivyopata taarifa tukatoka Dodoma kuja kufatilia na kwenda shuleni kwao na kiukweli taarifa tulizozipata shuleni zilikua haziridhishi kutokana na mazingira tuliyoyakuta”
“Wakati tunafatilia kwa kushirikiana na Shule na watu wengine na kituo cha Polisi cha Himo tukawa tumepata taarifa kwamba kuna Mwili uliokotwa mtoni karibia na shule ya Scolastica” – Makundi
Polisi Kilimanjaro bado inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na inamshikilia Mkuu wa shule hiyo ya Scolastica, endelea kuwa karibu na AyoTV na millardayo.com kupata taarifa kamili
POLISI KILIMANJARO KUHUSU KUPIGA MABOMU MANNE MSAFARA WA LOWASSA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI