Familia ya mtoto Paula Teixeira imeelezea mateso inayopitia na mtoto wao huyo ya kumuuguza kwa ugonjwa unaoweza kuchukua maisha yake muda wowote anapopata usingizi na kulala.
Inaelezwa kuwa ugonjwa huo ujulikanao kama Ondine Syndrome ni adimu na unaathiri watu 1000 hadi 2000 duniani ambao kwa kawaida huweza kuziba pumzi ya mgonjwa husika pindi tu anapolala usingizi na hivyo inahitaji mtu awepo macho muda wote mgonjwa anapokuwa amelala ili kulinda usalama wake.
Mama wa mtoto Silvana ameeleza kuwa mwanaye huyo mwenye miaka 3 ameishi maisha hayo tangu amezaliwa, na ndivyo itakavyokuwa kwa maisha yake yote, ambapo kitu pekee kinachoendelea kulinda uhai wake ni mashine ya hewa ya oxygen,
Baba wa mtoto huyo Roberto kwa upande wake amesema huwa kwa kawaida yeye na mkewe wanalala kwa zamu ili mmoja wao awe macho kumwangalia mtoto na kuhakikisha mashine yake ya kupumulia inafanya kazi vizuri, lakini hata hivyo bado wanakuwa na wasiwasi muda wote kuhusu usalama wa mtoto wao.
Ulipitwa na hii? Ruge aongea kuhusu FIESTA Dar kuisha saa 6 usiku