Habari nzuri ya kuanza nayo wiki ni hii ya BancABC ambao kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili watatoa huduma ya bima ya afya itakayofaidisha watoto 100 ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ndio ametoa baraka zake huduma hii mpya ya BancABC na Hospitali ya Muhimbili na kusema mradi huo utaenda sambamba na malengo ya Serikali kuhakikisha zinapatikana huduma za afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
“Natoa wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa kuwafungulia watoto wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha taslimu pale mtoto anapougua.” – Ummy Mwalimu