Habari zilizotufikia muda huu ni kwamba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaka Bahman wa Kampuni ya NAS na Wakala wa Kampuni ya Wallmark wakamatwe kwa kutaka kutoa bandarini DSM semitrela 44 kwa kutumia jina la Waziri Mkuu ili wasilipe kodi.
Ametoa maagizo hayo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamanda Simon Sirro pindi alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na hatimaye kupata taarifa ya mfanyabiashara huyo aliyepanga kutapeli Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Ulipitwa na hii? Ugeni wa Raza kwa Waziri Mkuu Majaliwa leo
BUNGENI: MBOWE VS MAJALIWA KUHUSU SHAMBULIO LA LISSU